Hekaheka ya leo February 19, inatokea Vingunguti inahusu mwanamke ambaye amekuwa na tabia ya ulevi wa kupindukia.
Mwanamke huyo amekuwa akimwacha mtoto wake mchanga bila kumnyonyesha, hii iliwakera majirani na kuamua kumpiga mwanamke huyo huku yeye akijitetea kwamba maisha yamemshinda ndio maana amekuwa mlevi.
Ndugu zake wamesema ulevi wake ulianza tangu akiwa mjamzito, ameendelea kufanya hivyo mpaka sasa na walipojaribu kumshauri aliwajibu vibaya ndio maana wakaamua kumpiga na kumpeleka kituo cha Polisi kumfungulia mashtaka.
Bonyeza play hapa ili kuisikiliza Hekaheka ya leo.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook