HekaHeka

Mume kasimulia alivyodanganywa na mkewe kwamba ni mjamzito kwa zaidi ya mwaka mmoja >>> #Hekaheka (Audio)

on

Hekaheka III

Wiki iliyopita kulikuwa  na Hekaheka iliyotokea Hospitali ya Mwananyamala Dar.. mwanamke mmoja akakamatwa  akiwa kwenye pilika pilika za kutaka kuiba mtoto mchanga kati wa watoto waliozaliwa huku akidanganya ndugu zake na mumewe pia kwamba kajifungua mtoto njiti !!

Mama mkwe na Muuguzi wa Hospitali hiyo walisimulia wiki iliyopita jinsi ambavyo ishu yote ilivyokuwa mpaka wakamgundua kwamba sio kweli kwamba amejifungua na alikuwa na mpango wa kuiba mtoto.

Mume wa mwanamke huyo amesema ndani ya mwezi mmoja baada ya kuanza uhusiano wao mwanamke akawa analalamika kwamba ni mjamzito lakini hakuwahi kuona dalili yoyote ya kuona tumbo kuongezeka ukubwa kuonesha ujauzito.. akawa anaenda clinic Magomeni lakini hakuwahi kuongozana nae.

Jamaa amesema kwamba alijitahidi sana kumhudumia kwa zaidi ya mwaka mmoja akijua kwamba mkewe ni mjamzito… baada ya kutokea ishu ya kukamatwa kwa mke wake jamaa anasema aliumia sana, hajaenda kumuona Polisi tangu alivyokamatwa na hana mpango kuendelea nae kama kesi ikiisha.

Hapa iko sauti ya mume akisimulia ishu hiyo kwenye #Hekaheka

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments