Kwenye hekaheka ya leo tukio limetokea Dar es Salaam, ambapo mzee mmoja amefanyiwa vitendo vya kikatili na vijana ambao alikwenda nao kunywa pombe.
Mzee huyo amesimulia ilivyokuwa, amesema siku chache zilizopita alikwenda kunywa pombe karibu na kwenye kibanda chake akiwa na baadhi ya vijana.. baadaye pombe zilimzidia..kesho yake asubuhi alikutwa kwenye kibanda chake akiwa hajiwezi na kukimbizwa Hospitali ya Amana, ambapo alipokelewa na vipimo kuonesha aliingiliwa kwa nguvu kinyume na maumbile.
Jirani yake ambaye alimsaidia amesimulia kwamba aliamka asubuhi na kukuta Mzee huyo akiwa na hali mbaya.
Kati ya Vijana ambao wanahisiwa kufanya kitendo hicho, amekamatwa na anashikiliwa kituo cha Polisi Stakishari wakati upepelezi wa Polisi ukiendelea.
Sikiliza tukio zima hapa….
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa, muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE