Kama umekuwa mfatiliaji wa stori za Magazetini wiki iliyopita kulikuwa na stori kubwa ambayo ilitawala sana kuhusu ishu ya ripoti za vipimo vya DNA kuwa kati ya walioenda kupima DNA imeonesha 49% ya watoto wanalelewa na baba ambao sio baba wazazi.
Baba wa mtoto huyo amesimulia kwamba hakupendezwa na kitendo cha dada mmoja anayeuza duka la dawa kumwambia zaidi ya mara moja kwamba mtoto anayemlea sio wa kwake !!
Kilichomkasirisha zaidi akaamua kumpiga mke wake ilikuwa ni bahati mbaya mtoto alichomwa na pasi wakati baba ananyoosha, mtoto huyo akasema ‘ndio maana sio baba yangu‘ !!
Baba akahisi kuna ukweli, kwa hasira akampiga mkewe huku akilazimisha waende kupima DNA Muhimbili ili wajue ukweli, kwa bahati nzuri majirani wakaingilia kati ugomvi huo… Geah Habib ameipata stori yote kwenye Hekaheka na nimeirekodi kukusogezea yote hapa.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE