Baada ya stori za muda mrefu kuhusu kiungo wa kimataifa wa Rwanda anayekipiga katika klabu ya Yanga Haruna Niyonzima, uongozi wa klabu hiyo December 28 umetangaza maamuzi mapya baada ya awali kutangaza kumsimamisha kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu.
Yanga wamefikia maamuzi ya kuvunja mkataba na kiungo huyo, baada ya kukaa na kufikiria kwa kina kutokana na tabia ya kiungo huyo kuwa kila anapokwenda kwao kucheza timu yake ya taifa ya Rwanda, huwa anachelewa kurudi bila sababu za msingi na wala taarifa rasmi.
Baada ya Yanga kutangaza maamuzi hayo kwa kile wanachokidai kuwa mchezaji huyo ameshindwa kuheshimu mkataba wake, Yanga wanadai fidia ya dola 71000 kama fidia ya kuvunja kwa mkataba huo, kwani wanadai mwenye makosa ni Haruna Niyonzima. Kiungo huyo wa kimataifa wa Rwanda alikuwa na mkataba na Yanga hadi mwaka 2017.
CHANZO CHA HII STORI: Shaffihdauda.com
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.