Kwenye Hekaheka ya leo Geah Habib amezungumzia kuhusu yule mtoto ambaye alikutwa amepigwa sana eneo la Mbezi Beach na kulazwa ICU..mtoto huyo ameruhusiwa kurudi nyumbani lakini hali yake bado si nzuri sana na upande mmoja amepooza..madaktari wamesema atapona taratibu sana.
Kingine ni kuhusu yule mtoto aliyekuwa akipata manyanyaso maeneo ya vingunguti kwa kupigwa na mama anayedaiwa ni shangazi yake..baada ya tukio hilo yule mtoto alichukuliwa ili kuwa katika mikono salama lakini kibaya zaidi shangazi alitoa namba ya baba yake ambaye ni kaka yake lakini inahofiwa alitoa namba ambayo si ya kweli.
Baada ya kufuatilia Polisi ili kupata namba za wazazi wake, kuna taasisi ya MKAKATI inayohusika na haki za watoto ilifuatilia habari hii baada ya kuisikiliza kupitia Hekaheka..Meneja wa taasisi hiyo amesema wao pia walipewa namba za uongo, ikabidi walifuatilie kwa kina na sasa shangazi wa mtoto huyo amerudishwa polisi na mtoto yupo chini ya taasisi hiyo.
Pia wamezungumzia mwendelezo wa yule baba aliyefanyiwa vitendo vya kihuni na vijana wa mtaani kwake baada ya kumwingilia kinyume na maumbile na kupelekea kulazwa hospitali ya Amana..hali yake inasemekana si nzuri na amehamishiwa hospitali ya Taifa Muhimbili na anatakiwa kufanyiwa upasuaji kwa mara nyingine.
Msikilize Geah Habib akizungumzia mwendelezo wa Hekaheka hizo…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE