Habari za Mastaa

Baada ya kimya kingi, T-Pain atangaza ujio wa album yake mpya; ‘Stoicville: The Phoenix’! (Video).

on

Mara ya mwisho umesikia T-Pain katoa album ilikuwa ni lini? Siku nyingi… Amini, usiamini imepita miaka 4 toka msanii huyo aachie album yoyote,  na mashabiki wake wengi wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefru sana ujio mpya wa msanii huyo mwenye midundo ya Crunk Music kwenye game ya muziki.

T-PAIN5

Nina good news ya kushare na wewe mtu wangu, T-Pain hivi karibuni ametimiza miaka 30 na kusherekea siku yake ya kuzaliwa msanii huyo aliwatangazia mashabiki wake kupitia page yake ya Twitter kuwa wategemee album yake mpya iliyopewa jina la Stoicville: The Phoenix tarehe 11 December mwaka huu!

T-PAIN

Kwenye interview moja aliofanya na moja ya online Tv za Marekani, Rap-Up TV, T-Pain aliulizwa tutegemee nini safari hii kutoka kwenye album yake mpya ambayo itakuwa album yake ya kwanza ndani ya miaka 4… T-Pain alikuwa na haya ya kusema…

T-PAIN2

T-Pain.

>>> “Ni album mpya ya T-Pain sio T-Pain mpya, hakuna kipya sana zaidi ya mimi kuwa original na kufanya kile kinachotoka moyoni, sijaribu kutengeneza hit album, nimeshavuka stage hiyo kwani nimeshafanya hivyo mara nyingi… sasa hivi nasukumwa sana kutengeneza muziki ambao nauamini, ni suala la mimi kuwa huru zaidi kuliko hapo mwanzoni! <<< T-Pain.

Unaweza pia ukamsikiliza T-Pain kwenye hii video hapa chini mtu wangu.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments