Wiki iliyopita baadhi ya vyombo vya habari viliandika stori ya mwanafunzi mmoja wa Shule ya Msingi Kunguru iliyopo Goba, Dar es salaam kupandisha mapepo huku yakitaja kutumwa na mwalimu wake yakidai yanampenda.
Leo timu ya HekaHeka imepiga hodi nyumbani kwa wazazi wa mtoto huyo aitwaye Modesta na kuzungumza naye ambapo alikiri kuwa mwalimu huyo alikua akimsumbua siku nyingi kuwa anampenda lakini kadri siku zinavyokwenda amekua akimchukia kila siku bila kujua sababu ni nini.
Mama wa mwanafunzi huyo amesema ni kweli mtoto huyo amekua na tatizo la kupandwa na mashetani huku akitaja kuwa mwalimu wake ndiye kawatuma na kudai anampenda lakini hakuwa na wasiwasi kwa kuwa ni mwalimu wa kike..amesema wamezunguka katika nyumba za ibada na kuombewa lakini hakuna mabadiliko yoyote mpaka sasa.
Mwalimu huyo ambaye ni wa jinsia ya kike amesema ndio kwanza anamsikia huyo mtoto leo..amesema ni kweli yupo karibu naye kama ilivyo kawaida,,yeye ameokoka na anaamini Mungu ndiye atakayemsimamia,,amesema wataabika wote wanaomtuhumu kwa kuwa yeye haamini mambo hayo.
Wasikilize hapa mwanafunzi, mama yake pamoja na mwalimu anayetuhumiwa wakizungumza na Geah.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos