Kwenye Hekaheka ya leo inahusu mwanamke aliyejifungua mtoto kisha dokta kuMngangania akidai hajalipwa fedha zake za matibabu.
Msamaria mwema aliyeshuhudia tukio hilo amesema mama wa mtoto alipanga na dokta kuitoa mimba baada ya kupewa na mwanaume mwingine huko Afrika Kusini alipokua akisoma huku akiwa na mchumba aliyemwacha Tanzania.
Aliporudi alitaka kuitoa na kukubaliana na dokta lakini tayari ujauzito wake ulikua mkubwa na ikabidi ajifungue lakini cha kushangaza dokta alimng’ang’ania mtoto wake aliyemwachia kwa muda wakati alipokwenda kuripoti nyumbani kwao na aliporudi alitaka ampe hela nyingi tofauti na walivyokubaliana.
Baada ya kumchukua mtoto dokta alimpeleka kwa msamaria mwema na akakubali kumlea lakini baada ya miezi michache alikwenda kumchukua na hakuweza kumrudisha tena mpaka sasa huku mama wa mtoto akimtafuta mtoto wake hadi leo bila mafanikio.
Msikilize hapa kwenye Hekaheka….
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos