Hekaheka ya leo inatokea Mbeya baada ya dada mmoja kupigwa sana na wifi yake ambaye ni mdogo wa mume wake kwa madai kuwa anamtafutia mume wake wanawake.
Mpaka sasa dada huyo amealazwa hospitali baada ya kuwa na majeraha makubwa. mbali na na dada huyo pia mama mkwe naye alipigwa hadi kuzimia wakati akiamua ugomvi huo wote wakituhumiwa kuharibu ndoa ya mwanamke huyo.
Shuhuda wa tukio hilo alisema tukio la kupigwa kwa dada huyo lilitokea baa ambapo mwanamke huyo alichukua chupa ya bia na kuivunja kisha kumkwangua nayo sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha makubwa.
Mpaka sasa mwanamke huyo anashikiliwa na Polisi huku aliyejeruhiwa akiwa bado amelazwa hospitali.
Ikilize hapa…
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.