Team ya Hekaheka leo ilikua eneo la Ununio nje kidogo ya jiji la Dar es salaam baada ya kupigiwa simu na watu kuhusu jirani yao ambaye alikuwa anakula kupita kiasi, kitu ambacho si cha kawaida.
Mwenyewe amesema anaona ni kipaji alichojaliwa na Mungu kwa kuwa na uwezo wa kula zaidi ya mtu wa kawaida..anasema kwa siku anamaliza kilo nne akimaanisha asubuhi anatumia kilo moja ya mchele, mchana unga kilo moja na jioni hivyo hivyo.
Anasema asubuhi akishindwa kula wali basi hula chapati 25 au maandazi 50, pia ana uwezo wa kumaliza soda 15 kwa wakati mmoja..na humfanya kuweza kufanya kazi yoyote ambayo atapata kwa siku hiyo.
Msikilize mwenyewe hapa akihojowa na Geah Habib…
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.