Kuna mama alimchukua mtoto wa jirani yake kutoka kijijini kwao Dodoma na kuja nae Dar es salaam akiahidi kumsomesha kama alivyoahidi kwa wazazi wa mtoto huyo.
Mtoto huyo mwenye miaka tisa baada ya kufika Dar alianza kufanya kazi zinazomzidi umri ikiwa kuchota maji kila siku pamoja na kuamshwa usiku kufanya kazi za usafi.
Team ya Hekaheka ilipata taarifa na kuamua kufunga safari hadi kwa mama huyo maeneo ya Mikocheni na kusimuliwa na majirani jinsi mtoto huyo alivyokuwa akifanya kazi bila kusomeshwa kama alivyoahidiwa mwanzo.
Stori kamili isikilize hapa kwenye Hekaheka ya leo…
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.