July 12 2016 Kupitia Hekaheka ya Clouds FM, Geah Habib ametuletea hii hekaheka kutokea Tandale Hospitali Dar es salaam ambapo mgonjwa aliyetoka nje ya hospitali na kukaa nje ya hospitali na akalala nje usiku kucha, mashuhuda wanasema hospitali walipopewa taarifa hawakujali.
Mashuhuda wanadai kuwa alishindwa kuhudumiwa kwa sababu alikuwa hana shilingi 2000 ya kadi na mpaka anakata roho alikuwa nje ya hosptali hiyo, millardayo.com imekurekodia full stori kutoka kwenye HekaHeka ya leo.
Mmoja wa mashuhuda amesema kuwa……….>>>’kaja toka jana kaingia ndani baada ya kuingia ndani kwa kuwa alikuwa hajiwezi alivyotoka akafikia akakaa hapa, basi alipofikia akalala mpaka leo asubuhi, tukawa waoga, tukaenda kituo cha polisi tukatoa taarifa, akaja polisi akamwangalia nae akaondoka, mwenyekiti akarudi tena nae akaondoka, mpaka inafikika saa 6;30 akawa anang’ata ulimi anakufa’
Kuisikiliza full story, bonyeza play hapa chini
ULIKOSA MATANO YA KUFAHAMU BAADA YA DC KINONDONI KWENDA HOSPITALI YA M/NYALA USIKU AKIJIFANYA MGONJWA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO