Leo July 11, 2017 Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, HESLB imetoa taarifa yake kuhusu hali ya urejeshaji wa mikopo ya wanafunzi walionufaika na mikopo hiyo ambapo kiasi cha Tsh. Bilioni 13,738,911,171.54 kimerejeshwa kutoka kwa mnufaika mmoja mmoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo Abdul-Razaq Badru ameeleza kuwa idadi ya waliojiajiri wamejitokeza kwa hiyari yao wenyewe kurejesha mikopo waliyopewa wakati wakiwa masomoni.
Zaidi ya Tsh Bil 13.7 zimerejeshwa kutoka kwa walionufaika na mikopo ya elimu ya juu, waliojiajiri wamejitokeza kwa hiyari kurejesha mikopo. pic.twitter.com/K5NPU8tE66
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Asilimia 65 ya kiwangi cha mikopo iliyokusanywa kimetoka kwenye sekta ya umma na asilimia 35 kwenye sekta binafsi' – Bodi ya Mikopo pic.twitter.com/JN8ybjkPgh
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Kuanzia July 2015 hadi June 2016 Bodi ya Mikopo imetoa Tsh. Trilioni 2.5 kwa wanafunzi 330,801, idadi ya wanafunzi waliokopeshhwa ni 379,179 pic.twitter.com/yPipfn3BcC
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
VIDEO: Ulipitwa na uchambuzi wa Magazeti ya leo July 11, 2017? Bonyeza play kutazama hapa chini.