Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Mashabiki wa Man United wamjia juu staa wa Tottenham Hotspurs

on

Mashabiki wa club ya Man United wameonekana kuchukizwa mitandaoni kufuatia tukio la kukanyagwa kwa mchezaji wa timu ya Man United Daniel James dhidi ya Moussa Sissoko wa Tottenham Hotspura huku akiwa hajaoneshwa kadi yoyote kama ishara ya kuadhibiwa.

Kwa sasa club za Man United na Tottenham zipo Shanghai China kucheza mechi za kirafiki za maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu England, hivyo katika mchezo kati ya Tottenham dhidi ya Man United uliyomalizika kwa Man United kupata ushindi wa 2-1, Moussa Sissoko alimkanyakaga James pembezoni mwa kifua wakati wa mchezo huo wakiwa katika kibendera cha kona.

Kitendo ambacho mashabiki wa Man United wamekitafsiri kama cha makusudi na sio bahati mbaya kama wanavyodhani baadhi ya watu, Ma United wanajiandaa Ligi Kuu England ambapo wataanza mchezo wao wa kwanza August 11 dhidi ya Cheslea wakati Tottenham nao wataanza mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu England dhidi ya Aton Villa August 10 2019 wakiwa nyumbani.

VIDEO: Mzee Shaweji Kaeleza Kwa Nini hawataki kutoa hati kwa MO Dewji

Soma na hizi

Tupia Comments