Leo March 5, 2018 Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amemfuta kazi Inspekta mkuu wa polisi, Kale Kayihura na waziri wa Ulinzi, Henry Tumukunde.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Museveni amesema: ” Kwa uwezo wa mamlaka niliyopewa kikatiba, nimemteua Jenerali Elly Tumwiine kama waziri wa usalama. Nimemteua pia bwana Okoth Ochola kama afisa mkuu wa polisi. Niabu wake atakuwa ni Brigedia Sabiiti Muzeei.”
Generali Kayihura, alishiriki katika vita vilivyomsaidia rais Museveni kuingia madarakani mwaka 1986, lakini amekabiliwa na shinikizo kwa kushindwa kukabiliana na ukosefu wa hali ya usalama.
Zaidi ya wanawake 20 wameuawa katika visa vya mauaji ambavyo havijatatuliwa katika maenoe yanayouzunguka mji mkuu wa Kampala, na katika miezi mitatu iliyopita raia watatu wa kigeni pia wameuawa.
DR TULIA TENA MBEYA LEO “YAWEZEKANA HATUWAFIKII KWA WAKATI”