Michezo

Mashabiki wa Arsenal wamepewa onyo na UEFA kuelekea fainali ya Europa League

on

Baada ya kufahamika kuwa kiungo wa kimataifa wa Armenia anayeichezea club ya Arsenal ya England Henrikh Mkhitaryan kuthibitika kuwa hatosafiri na timu hiyo kuelekea Azerbaijan katika mji wa Baku kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Europa League kati ya Arsenal dhidi ya Chelsea.

Mashabiki wa Arsenal wanadaiwa kuwa wamepanga kuingia na mabango kwa ajili ya kupinga Azerbaijan kusababisha Mkhitaryan kuhofia kuingia katika taifa hilo, Mkhitaryan ameshindwa kuiingia Azerbaijan kwa kuhofia usalama wake kutokana na tofauti ya kisiasa iliyopo kati ya taifa lake la Armenia dhidi ya Azerbaijan.

UEFA wamemthibitishia usalama Mkhitaryan lakini Arsenal wameona ni bora wamuache, hivyo mashabiki wa Arsenal wamepewa onyo wasijekujaribu kuingia na mabango ya kupinga chochote, kama Arsenal watafanya hivyo wataingia katika mkubo wa Celtic waliowahi kupigwa faini ya pound 20000 kwa mashabiki wake kuingia na bango lenye maneno yasio faa.

Mapokezi ya Sevilla Tanzania waliokuja kukipiga na Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments