Timu zinazoshiriki michuano ya SportPesa Cup zilianza kuingia Dar es Salaam mwishoni mwa wiki huku michuano hiyo ikitarajiwa kutimua vumbi wiki hii. Michuano hiyo ambayo imekuwa ikifuata umati mkubwa wa mashabiki ukanda huu wa Afrika Mashariki wiki itashuhudia timu 8 zikishiriki, huku Kenya na Tanzania kila moja ikiwakilishwa na timu nne
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas alisema kuwa matayarisho ya michuano hiyo awamu ya tatu yamekamilika huku timu zikiwa zimeanza kuingia Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. SportPesa Cup awamu ya tatu inatarajiwa kuanza Jumanne ya wiki hii.
Kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) wamekubaliana kutoza kiingilio cha chini ili kuweza kuvutia mashabiki wengi. Mashabiki wa mpira wa miguu kutoka Tanzania na Ukanda huu wa Afrika Mashariki kwa jumla watalipa TZS 10,000 kwa VIP A,huku VIP B na VIP C wakilipa TZS 5,000 na mzunguko TZS 2,000 kwa mechgi za robo fainali.
Wakati huo huo, mchezaji wa zamani wa timu ya Everton FC na Balozi wa klabu hiyo Steven Pienaar anatarajiwa kutua jijini wiki hii kwa nia kuwatiaa hamasa wachezaji chipukizi hapa nchini(BOMBOM FC). Wakati wa ziara yake, mchezaji huyo atafanya mazoezi ya pamoja na timu ya taifa ya U17 ambayo inajiandaa kwa ajili ya michuano ya AFCON ambayo inatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam baadae mwaka huu.
Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas alisema kuwa ziara ya Steven Pienaar hapa nchini ni moja ya mikakati ya muda mrefu ya SportPesa ya kukuza mpira wa miguu hapa Tanzania. Kwa muda mrefu SportPesa imekuwa na mikakati dhabiti ya kukuza mpira wa soka hapa nchini na kwa sababu ndio imeifanya timu ya Everton FC kushirikiana na SportPesa.
VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”