Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr Mwigulu Nchemba ametoa mabati 210 na cement mifuko 100 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati na mabweni ya wanafunzi katika kata ya Mtoa katika Jimbo la Iramba Magharibi kusaidia kupunguza adha iliyopo.
Inaelezwa kuwa inawalazimu wananchi wa eneo hilo kuvuka mto mkubwa kufata huduma ya afya umbali wa zaidi ya Kilimota 10.
Waziri Nchemba ameeleza kukerwa na jengo kukaa muda mrefu bila kumaliziwa hivyo ameamua kutoa mabati hayo na kuchangia Shilingi Milioni Moja na Nusu kwa ajili ya ununuzi wa mbao ili ujenzi uanze mara moja na ukamilike ili huduma zianze kutolewa ndani ya mwaka huu.
Aliongeza kwa kusema kuwa wakati wa masika baadhi ya maeneo ni ngumu sana hata magari kufika kutokana na mito kujaa maji na barabara kuwa na utelezi na kufanya gari au watu kushindwa kupita kufata huduma za afya.
“Naomba radhi watu wote…..” – LUKUVI
Maamuzi ameyachukua Naibu Waziri wa Elimu kwa Mwalimu Mkuu