Ligi kuu ya Uhispania imeendelea leo baada ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa kumalizika, Real Madrid walisafiri mpaka jijini Barcelona kwenda kucheza na Espanyol.
Mchezo uliopigwa katika dimba la Cornella El Plat umeshuhudia mwanasoka anayeshikilia taji la uchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo akifunga magoli 5 katika mchezo uliomalizika kwa Real Madrid kushinda 6-0.
Ilimchukua Cristiano Ronaldo dakika 20 tu kufunga hat trick katika dakika ya 7, 17 na 20, kabla ya Karim Benzema hajafinga goli la 4 katika dakika ya 28 na hivyo kupelekea Madrid kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa 4-0.
Kipindi cha Ronaldo akaongeza magoli mawili katika dakika ya 60 na 80 ya mchezo huo na hivyo kukamilisha ushindi wa 6-0
Timu zilipangwa hivi
Espanyol: Lopez, Arbilla, Alvaro, Ciani (Paco Montanes 46), Duarte, Victor (Joan Jordan 64), Javi Lopez (Canas 46), Alvarez, Salva, Gerard, Caicedo
Substitutes not used: Bardi, Juan Fuentes, Raillo, Sylla
Booked: Alvaro, Canas
Real Madrid: Navas, Carvajal, Pepe, Ramos (Varane 74), Marcelo, Casemiro, Modric (Kovacic 55), Isco, Bale, Ronaldo, Benzema (Vazquez 62)
Substitutes not used: Casilla, Kroos, Arbeloa, Jese
Scorers: Ronaldo 7, 17 pen, 20, 61, 80; Benzema 28