Mwamuzi aliyechezesha mchezo wa ligi kuu ya Hispania kati ya Athetico Bilbao VS Real Madrid na kumtoa kwa kadi nyekundu mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo wikiendi iliyopita amesimamishwa.
Kamati ya marefa nchini Spain imemuadhibu refa Miguel Angel Ayza Gamez kwa kumsimamisha kwa mwenzi mzima na huku akiondolewa katika isti ya marefa watakaochezesha mechi za Real Madrid zilizobakia msimu huu.
Refa huyo alitoa kadi nyekundu kwa Ronaldo ambayo ilionekana kuwa na utata mkubwa jambo lilopelekea malalmiko kutoka kwa klabu ya Real Madrid.
Kutokana na kadi hiyo nyekundu ya moja kwa moja Ronaldo amefungiwa kucheza mechi tatu na atazikosa mechi tatu zijazo za timu yake dhidi ya Villarreal, Getafe na Elche.
Hata hivyo kufungiwa kwa refa huyo aliyemsababishia kufungiwa huko kunaweza kuipa nguvu Real Madrid kukata rufaa dhidi ya kadi hiyo ya Ronaldo.