Mtoto wa miaka 12 ameshangaza watu baada ya kutoroka wazazi wake na kusafiri peke yake kwenda mapumzikoni kutoka Sydney nchini Australia hadi Bali Indonesia.
Mtoto huyo aliamua kufanya hivyo baada ya wazazi wake hao kuahirisha safari hiyo ambayo walikuwa wamepanga waende na mtoto wao huyo.
Mzee Majuto azidiwa, arudishwa tena Hospitali kwa tatizo jingine
Mtoto huyo anadaiwa kutafuta ndege kwenye mtandao na kufanya ‘booking’ mwenyewe na kuondoka bila wazazi wake kujua huku akitumia passport na kitambulisho chake cha shule airport.
March 17, 2018 mtoto huyo alikutwa kwenye kisiwa hicho cha Bali ikiwa ni siku tisa baada ya wazazi hao kuripoti polisi juu ya kutoonekana kwa mtoto wao.
ACT Wazalendo wamezungumza kufichwa kwa Zitto Kabwe