Leo March 5, 2018 kutoka Iramba katika Jimbo la Dr. Mwigulu Nchemba Wachimbaji wa madini wameombwa kusaidia kupunguza tatizo la mimba kwa wanafunzi wa kike kwa kusaidia shughuli za maendeleo ya ujenzi wa hosteli za wasichana katika shule za sekondari nchini.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Ester Yona wakati akipokea mabati 360 yaliyotolewa na Mgodi wa Shanta tawi la Singida kusaidia jitihada za Mbunge wa Jimbo hilo Dr Mwigulu Nchemba ambaye ameanzisha ujenzi wa hosteli za wasichana katika kila shule ya sekondari jimboni humo.
Ester amesema tatizo la mimba kwa wanafunzi wa kike bado lipo jimboni humo na wengi wanaacha masomo na wengine kuwa na ufaulu wa chini jambo lililofanya Waziri Mwigulu aanzishe ujenzi huo wa hosteli ili kupunguza kasi ya tatizo hilo la mimba kwa wanafunzi.
Ameongeza kusema kuwa msaada waliopata wa bati 360 watapeleka katika majengo ambayo yapo tayari kwa kupauliwa ambayo yapo katika Kata za Kyengege na Ntwike ambapo wamepanga ifikapo mwezi May 2018 yaanze kutumika.
Naye meneja mkuu wa Singida Shanta mining Engineer Filbert Rweyemamu amesema wameamua kuunga mkono juhudi za Waziri Mwigulu za kutatua changamoto hiyo ya mimba kwa wanafunzi kwa kutoa vifaa hivyo vyenye thamani ya Shilingi Milioni 9.
“Nipeni ripoti kamili ya ukarabati hapa, sijarizika nao” Naibu Waziri wa Elimu
Anaedai kugundua Tanzanite aomba kukutana na JPM