Staa wa Sweden aliyekuwa anaichezea Man United ya England Zlatan Ibrahimovic ametumia style ya kipekee kuutangazia umma kuwa kwa sasa anaenda kucheza soka Marekani katika club ya LA Galaxy inayoshiriki Ligi Kuu Marekani MLS.
Unaambiwa Zlatan amelipia ukurasa mzima wa gazeti la LA Times na kuandika tangazo maalum kuhusu ujio wake mpya katika club hiyo, ukurasa huo umeandika stori kuhusu ujio wa Zlatan na kutoa picha ya Zlatan akiwa amevaa jezi za LA Galaxy.
Taarifa hiyo iliyotolewa na gazeti la LA Times Sport imeandika kuwa kwa sasa Zlatan Ibrahimovic anawasili katika club hiyo likiwa ni jina kubwa zaidi ya David Beckham aliyejiunga timu hiyo miaka kadhaa iliyopita, Zlatan anaondoka Man United baada ya kuitumikia katika game 53, kafunga magoli 29 akitoa assist 10.
Hivi ndio Simba walivyotoka sare ya 2-2 dhidi ya Al Masry