Ukaribu wa Wizkid na mwanamitindo maarufu kutokea London Naomi Campbell unazidi kuweka alama ya viulizo kwa baadhi ya mashabiki hii ni baada ya kuonekana pamoja tena kwenye sherehe za utoaji wa tuzo za GQ Men of the Year 2018.
Sherehe hizo zilifanyika katika ukumbi wa Tate Modern jijini London usiku wa September 5,2018 ikiwa wawili hao walionekana pamoja wakati wakuingia na baadae wakiwa wanatoka lakini tetesi zinadai kuwa hawakuonekana kwenye red carpet pamoja wakati wa kuingia.
Naomi Campbell na Wizkid ukaribu wao ulianza kuonekana miezi miwili iliyopita baada ya kutembea pamoja kwenye maonyesho ya mavazi ya Dolce & Gabanna yaliyofanyika Milan Italy na tokea hapo wamekuwa wakionekana pamoja mara kwa mara.
Kutoka kwa Steve Nyerere “Tuna mkataba na Mungu”