Stori inayoshika headlines nchini Ethiopia ni ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu, na sasa ni siku mbili baada ya Waziri Mkuu Hailemariam Desalegn kutangaza kujiuzulu na serikali ya nchi hiyo imetangaza ‘hali ya tahadhari’ nchini humo.
Ethiopia Imetoa tangazo kupitia kituo cha Televisheni yake ya taifa na kueleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kukabiliana na mfululizo wa maandamano dhidi ya serikali ambayo yanaendelea na kusababisha uharibifu.
Inaelezwa kuwa mamia ya watu wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa ndani ya miaka mitatu ya machafuko yanayoendelea nchini humo.
Hali ya dharura ya miezi 10 ambayo ilimalizika mwaka jana imeshindwa kuzuia maandamano hayo, hususani baada ya kuachiwa huru kwa maelfu ya wafungwa wa kisiasa.
Polepole, Lukuvi na Musukuma kwenye kufunga Kampeni za CCM Siha
Lowassa ametaka athibitishiwe kama hawatomnyima kura Mgombea wa CHADEMA