Staa kutoka WCB Harmonize mchana wa December 28 ametembelea Kituo cha Watoto yatima cha EAGT kilichopo Mtwara Mjini kwa ajili ya chakula cha mchana ikiwa pamoja na kukabidhi misaada kituoni hapo. Harmonize kwenye safari yake hiyo ameongozana na mpenzi wake wa sasa Sarah, ambapo kabla ya kukabidhi misaada yao walianza kwa kuhudumia chakula kwa kila mtoto aliyefika, Usiku wa Dec 31 Harmonize anatarajia kufanya show yake kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona ambayo amepanga kumtambulisha rasmi mpenzi wake Sarah..
Staa wa Bongofleva @harmonize_tz akigawa chakula kwa watoto yatima wanaolelewa katika Kituo cha Kanisa la EAGT Rahaleo, Mtwara kama sehemu ya shukrani zake kwa jamii kwa mwaka 2017. #MillardAyoUPDATES. pic.twitter.com/tg3rNDNscp
— AyoTV (@AyoTV) December 28, 2017
Uliiona hii ya Wolper alivyofunguka kuachana na Harmonize? https://www.youtube.com/watch?v=a2rf74fBGCc&t=169s