Mara nyingi stori za aina hii huanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, baadae unaona RADIO na TV nazo zinaanza kuripoti ambapo April 9 2015 watu walianza kusambaziana picha za ajali iliyotokea Tanga, mabasi mawili ya abiria na gari dogo yamegongana, watu 10 wamefariki na wengine kujeruhiwa.. kabla siku haijaisha naipokea hii nyingine kutoka Morogoro.
Basi la Kampuni ya Happy Nation T 618 BDN lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Mbeya lilipata ajali hiyo eneo la Mikumi, Morogoro na taarifa za kwanza kuzipokea zilikua za watu wawili kufariki na wengine kujeruhiwa.
Chanzo cha ajali hakijafahamika, naifuatilia hii kwa ukaribu.. kitakachonifikia nitakusogezea hapa muda wowote mtu wangu.
#RIP kwa watu wetu waliofariki kwenye ajali hiyo, pole kwa waliopata majeraha pia.
millardayo.com ni sehemu yako utakapozipata zote unazozitaka, vichekesho, stori za siasa, muziki, michezo, ovies,nmagazeti,nvideompya na nyingine kubwa…. unawez kujiunga na mimi Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook