Bondia mtanzania Omar Kimweri ambaye anafanya kazi zake na kuishi nchini Australia Ijumaa ya August 31 2018 amewasili Tanzania akitokea Australia kwa ajili ya kumfuata kocha amuandae katika pambano lake.
Omar Kimweri licha ya kuishi na kufanya kazi nchini Australia ameamua kurudi nyumbani Tanzania kwa mwezi mmoja ili ajiandae na pambano huku akifundishwa na kocha Habibu Kinyogoli.
Pamoja na kuwa Australia kuwa ni moja kati ya nchi zilizoendelea katika michezo mbalimbali kuliko Tanzania na kuna makocha wa Boxing mahiri lakini Omar amesema kuwa anamuamini zaidi Habibu Kinyogoli kwa ajili ya kumfundisha kwa wiki moja kwa ajili ya pambano lake la mwisho.
Kitu Mzee Akilimali kaongea kuhusu stori za Yussuf Manji kurudi Yanga SC