Ndani ya wiki moja tumeshuhudia headlines nyingi kuhusu Marekani baada ya nchi hiyo kuhalalisha ndoa za jinsia moja, leo ninayo nyingine iliyofikia kutoka Msumbiji!!
Kwao tangu mwaka 1886 ilikuwa MARUFUKU kujihusisha na uhusiano wa jinsia moja, Jumatatu June 29 2015 Msumbiji wametangaza kuhalalisha na kukubali kuzitambua ndoa za jinsia moja.. kingine kilichohalalishwa Msumbiji ni ishu ya wanawake kutoa ujauzito.
Marekani zilifanywa sherehe kubwa baada ya kuhalalishwa ndoa hizo, Msumbiji hakuna sherehe yoyote iliyofanywa mpaka sasa hivi.

Kuna nchi hawataki kabisa kusikia biashara ya kuhalalisha ndoa hizo, Rais Mugabe ni mmoja ya Marais ambao hawajifichi kabisa kupinga, Sudan, Nigeria na Mauritania nako ukikamatwa hukumu yake ni kifo… Msumbiji imeamua hivyo japo inaonekana nchi nyingi za Afrika zinapinga kuzitambua ndoa na uhusiano wa jinsia moja.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.