Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe ameeleza jinsi alivyokutana na marehemu Dr.Reginald Mengi wakati akiwa mtangazaji wa ITV, huku akisema hadi Dr.Mengi anafariki dunia alikuwa msaada katika wilaya hiyo.
Pia DC Gongwe amesema mara ya mwisho kuzungumza na Dr.Mengi ni mwezi uliopita ambapo alimtani kwa kumuita Mheshimiwa DC.
Akizungumza na Ayo Tv na Millardayo.com, DC Gondwe amesema licha ya kuwa Dr.Mengi alikuwa na umri mkubwa lakini alikuwa na fikra za ujana kutokana na kujishughulisha katika mambo mbalimbali ikiwemo uwekezaji wa viwanda vya simu na magari.