Leo January 22, 2018 nyota wa zamani wa soka Duniani George Weah ameapishwa kuwa Rais wa Liberia katika sherehe iliyohudhuriwa na maelfu ya watu katika mji mkuu wa nchi hiyo Monrovia.
Sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi wa mataifa kadha pamoja na Mastaa wa soka duniani. Akihutubia baada ya kula kiapo, Weah amesema: “Nimekuwa katika viwanja vingi maishani, lakini sijawahi kuhisi hivi.”
“Nitafanya zaidi ya mchango ninaotarajiwa kutoa ili kutimiza matarajio yenu, lakini naomba nanyi mtimize matarajio yangu, siwezi kutimiza haya peke yangu.”– George Weah
VIDEO: MSIMAMO WA ACT WAZALENDO KUELEKEA UCHAGUZI WA FEBRUARY 17