Mashabiki wa Nipsey waonyesha hasira zao kwa kuanza kutoa michoro ya Rapper Kodak Black kwenye makumbusho ya wasanii wa muziki wa Trap nchini Marekani, hii ni kufuatia kauli yake ya utata juu ya mke wa marehemu Nipsey Hussle ambaye ni Lauren London.
Kodak alisema kwa sasa Lauren ni mjane hivyo kwa kuwa anampenda sana basi yeye atakuwa mwanaume anayemfaa na atamliwaza kwa mwaka mzima kwa sababu anaamini atakuwa akimlilia mume wake Nipsey kwa kipindi chote cha mwaka mzima aliyasema hayo kupitia insta Live.
Baada ya muda mchache Kodak alirudi tena insta Live na kuomba radhi kwa kauli hiyo lakini wakali kama The Game na T.I walionyeshwa kutopendezwa na kauli yake hiyo. Hata hivyo kituo cha redio cha Power 106 cha Los Angeles kilitangaza kutopiga muziki wake tena.
VIDEO: LULU DIVA KUOLEWA/ AROBAINI YA RUGE/ ALIKIBA AMUONYESHA MTOTO WAKE