Leo ilikua ni zamu ya Chato Geita kumtazama na kumsikiliza LIVE Mgombea Urais kwa ticket ya CCM Dr. John Pombe Magufuli akinadi sera zake kuomba kura za Urais kwenye uchaguzi mkuu wa October 2020 ambapo wakati akijinadi, moja ya alivyoviongea ni hili la kauli mbiu au misemo ya Wagombea wengine wa Urais.
“Sioni katika Wagombea Urais ambaye anaweza kufanya niliyofanya hata robo, huwezi kusema ‘mtakula ubwabwa’ wakati hata kwao haumtoshi huo ubwabwa, huwezi kuzungumza ‘mtakula bata’, hakuna vya bure hata Misaafu yote inazungumza asiyefanya kazi na asile”– asema Dr. Magufuli akiwa Chato leo.
“Nimefanya mengi kwa miaka mitano, nawaomba Watu wa Chato na Watanzania wote nipeni tena miaka mitano, sioni katika Wagombea wote wa Urais ambaye anaweza kutekeleza niliyofanya hata kwa robo, kama mnataka kujaribu jaribuni ,mtakuja kuniambia” -JPM
TAZAMA YOTE ALIYOYAONGEA KWENYE KAMPENI ZAKE ZA CHATO LEO KWA KUBONYEZA PLAY HAPA CHINI