Chama cha taifa cha wamiliki wa bunduki Marekani (NRA) kimeonekana kubadilisha msimamo wake na kuunga mkono udhibiti wa kifaa kinachotumika kwenye silaha za moto ambacho kinawezesha silaha kufyatua risasi kwa mfululizo kwa kujiendesha yenyewe.
Hii inafuatia tukio la mwanaume aliyejulikana kwa jina la Stephen Paddock aliyefyatua risasi kwa kutumia kifaa hiki na kuuwa watu zaidi ya 50 huku akijeruhi zaidi ya watu 500 waliokua kwenye tamasha mjini Las Vegas.
Rais Donald Trump amesema wanaangalia uwezekano wa kupiga marufuku kifaa hicho kijulikanacho kama ‘bump-stock’ ambacho huondoa haja ya mtu anayetumia bunduki isiyo na uwezo kamili wa kufyatua risasi mfululizo kutumia bega lake kuidhibiti bunduki wakati wa kufyatua risasi.
Ulipitwa na hii?Mahakama ya Kisutu imemuachia huru Askofu Gwajima