Leo December 2 2016 mahakama kuu kanda ya Dar es salaam imetoa maamuzi ya kesi ya kupinga baadhi ya vipengele vya sheria ya mitandao. Mahakama hiyo imesema vipengele vingi vipo sawa na vinaendana na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pamoja na maamuzi hayo mahakama hiyo pia imetamka kuwa kifungu cha 50 kimekiuka katiba ya Tanzania na hivyo imetaka kifanyiwe marekebisho ndani ya miezi 12.
Bonyeza Play kwenye video hii fupi hapa chini, wakili wa kujitegemea Gabriel Kambona ameutoa ufafanuzi kuhusu maamuzi hayo ya mahakama kuu kwenye kesi ya kupinga baadhi ya vipengele vya sheria ya mitandao.
VIDEO: Mwijage kazisoma taarifa za wawekezaji 6 wanaotaka kuondoka TZ, Bonyeza play hapa chini kutazama