Club ya Man United ya England baada ya kukaa na kumuangalia katika michezo 19 akiiongoza timu yao Ole Gunnar Solskjaer kama kocha wao wa muda, wameamua kumtangaza rasmi kuwa kocha wao mkuu wa kudumu.
Man United imeamua kumpa mkataba wa miaka mitatu Ole Gunnar Solskjaer kama kocha wao wa kudumu, awali Man United ilikuwa imemteua Ole Gunnar Solskjaer kama kocha wao wa muda kumrithi Jose Mourinho hadi mwisho wa msimu huu.
Solskjaer akiwa na Man United sasa amefanikiwa kuiongoza club hiyo katika michezo 19, amefanikiwa kushinda michezo 14, sare michezo miwili na amepoteza michezo mitatu, kama utakuwa unakumbuka vizuri Ole Gunnar Solskjaer aliwahi kuwa mchezaji wa Man United katika kipindi cha miaka 11 (1996-2007).
Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars