Alhamisi ya June 29, 2017 Rais wa Simba SC Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange Kaburu walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kusikiliza mashitaka yao.
Evans Aveva na Kaburu wameshtakiwa kwa makosa matano ambayo kwa mujibu ya sheria yanawanyima dhamana hivyo wamelazimika kwenda rumande hadi July 13 ambapo kesi yao itaendelea chini Hakimu Victoria Nongwa.
Makosa matano wanayotuhumiwa nayo viongozi wa Simba SC
1- March 5 2016 Evans Aveva anatuhumiwa kughushi nyaraka za kuidai Simba dola 300,000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 600.
2-March 16 zilitumika nyaraka za uongo kujilipa deni kupitia bank ya CRDB Azikiwe.
3- Kula njama na kutakatisha fedha kinyume cha sheria kiasi cha dola 300,000 za kimarekani.
4- Kosa la nne Evans Aveva anatuhumiwa kutakatisha fedha ambazo alizipokea kupitia bank ya Barclays tawi la Mikocheni.
5- Kaburu anatuhumiwa pia kumsaidia Evans Aveva kutakatisha fedha dola za kimarekani 300000 kupitia Bank ya Barclays tawi la Mikocheni.
Kwa mujibu wa sheria makosa ya kutakatisha fedha hayana dhamana hivyo Evans Aveva na Geofrey Nyange Kaburu watakuwa lumande hadi July 13.
VIDEO: All Goals Taifa Stars vs Lesotho June 10 2017, Full Time 1-1