Baada ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kuifunga Uganda 3-0 katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza AFCON 2019 na kufuzu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39, Rais Magufuli aliwaita wachezaji Ikulu Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapongeza na kuwapa zawadi wachezaji.
Rais Magufuli akiwa na wachezaji hao pamoja na bondia wa kitanzania Hassan Mwakinyo baada ya kumpiga bondia wa Argentina Gonzalez, Rais Magufuli ametangaza kutoa Tsh Bilioni 1 kwa ajili ya maandalizi ya fainali za AFCON U-17 zinazofanyika Tanzania mapema mwezi April.
Pamoja na hayo Rais Magufuli ametoa zawadi ya viwanja kwa wachezaji wote wa Taifa Stars na kuwaagiza wapatiwe viwanja hivyo makao makuu ya nchi Dodoma, mchezaji wa zamani wa Taifa Stars Peter Tino aliyefunga goli la Taifa Stars kucheza AFCON 1980, Rais Magufuli amempa Tsh Milioni 5 baada ya mchezaji huyo kusema kuwa hana cha kufanya kwa sasa.
MUHIMBILI JKCI NAO WATANGAZA NUSU BEI KWA USHINDI WA TAIFA STARS