Timu ya taifa ya Uganda jana ilitangaza kikosi cha wachezaji 46 ambao watachujwa kuelekea mchezo wao wa mwisho wa kukamilisha ratiba kwa upande wao wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika 2019 nchini Misri.
List ya wachezaji wa timu ya taifa ya Uganda katika majina hayo 46, wachezaji 15 wa wanaocheza Ligi za nje ya Uganda wamepita moja kwa moja na wataungana na timu wakiwa Cairo Misri kwa ajili ya Kambi wakati 31 wao ndio watachujwa na kubakia wachezaji 9 wataoungana na 15 kutimiza idadi ya wachezaji 24.
Wakiwa wanaelekea mchezo huo kucheza dhidi ya Tanzania ambayo inahitaji ushindi katika mchezo huo, Uganda katika list hiyo ya wachezaji wa kimataifa imemjumuisha pia mchezaji wa kikosi cha akiba cha wachezaji wa Borussia Dortmund ya Ujerumani ambaye pia ana asili ya Uganda Herbert Bockhorn.
Herbert Bockhorn kwa sasa anacheza nafasi ya beki wa kulia na amezaliwa Uganda lakini ni raia wa Ujerumani na Uganda, hivyo inaelezwa ameamua kuichezea Uganda kwa sababu anaamini hawezi kuwa na nafasi katika kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake