Kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji anayeichezea club ya Chelsea ya England Eden Hazard bado inaonekana hajabadili maamuzi yake moja kwa moja na kutangaza kubakia Stamford Bridge kwa misimu kadhaa mbele, Hazard anahusishwa kuwa anaweza akaihama Chelsea kwa miezi ijayo.
Hazard ambaye anahitajika na club ya Real Madrid ya Hispania, leo amenukuliwa akithibitisha kuwa tayari amefanya mazungumzo na club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa inayochezea na mastaa mbalimbali duniani kama Kylian Mbappe, Neymar na Cavani.
Hazard amethibitisha kuwa 50% kwa 50% kuwa anaweza akaondoka Chelsea au akabakia “Nabaki Chelsea nina mkataba hadi June 2019, kama sitaongeza mkataba basi kuna uwezekano wa mimi kuondoka lakini sioni kama naweza kuondoka Chelsea January, kipindi cha usajili cha majira ya joto naona uwezekano wa mimi kuondoka lakini pia inawezekana nikamalizia soka Chelsea”
“Nimefanya mazungumzo na PSG lakini sijavutiwa nao nilishasema toka awali kama nitarudi kucheza Ligue 1 basi nitarudi kucheza katika club yangu ya zamani Lille” Chelsea baada ya kufanikisha kumbakisha Kante Stamford Bridge sasa wanaimani watafanikiwa kwa Hazard waliyemsajili miaka 6 iliyopita akitokea Lille ya Ufaransa kwa pound milioni 32.
Watanzania waishio Afrika Kusini wamejipanga kuelekea Lesotho leo