Asubuhi ya October 11 2018 mfanyabiashara na bilionea kijana Afrika Mohamed Dewji ambaye pia ni muwekezaji ndani ya club ya Simba SC, ameripotiwa kutekwa na watu wasiojulikana na kupelekwa kusikojulikana.
Mohamed Dewji ametekwa akiwa nje ya Hotel Colessum Dar es Salaam akiwa anataka kuingia Gym kufanya mazoezi kama ilivyo kawaida yake, kufuatia taarifa hizo uongozi wa club ya Simba SC na benchi la ufundi la timu hiyo likiongozwa na kocha wao limearisha mazoezi leo kwa ajili ya kufanya maombi ya kumuombea MO Dewji.
“Uongozi wa klabu ya Simba kwa mashauriano na Benchi la Ufundi la klabu yetu, chini ya Kocha Mkuu Patrick Aussems limeamua kuhairisha mazoezi ya Timu leo, ili kutoa fursa kwa Wachezaji na Benchi la Ufundi kushiriki ipasavyo kwenye Dua na Sala kwa ajili ya kiongozi wetu MO”
“Tunawaomba tena na tena watanzania na wanoitakia mema nchi yetu..wasiache kumuombea uhai na uzima Bwana Mohammed Dewji..Insha’Allah kheri @moodewji 🙏🙏”
“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga