Mapya yaibuka kutoka kwa mpenzi wa zamani rapper Bow Wow, Kiyomi Leslie ambaye amefunguka kupitia ukurasa wake wa Twitter na kudai kuwa aliwahi kupigwa na mwimbaji huyo kipindi akiwa mjamzito hadi mimba kutoka.
Inaelezwa kuwa Kiyomi ameamua kumfungulia mashtaka Bow Wow kwa kosa hilo la kumpiga akiwa mjamzito na mpaka kufikia hatua ya kutoa malalamiko yake kwenye mitandao ya kijamii ambapo pia June 30,2019 aliandika nimekuwa nikijaribu kusonga mbele na maisha yangu na kuwa mtu wa kawaida lakini wanataka kunididimiza chini.
“Nina uhakika hatowaambia kuwa Polisi walimuita zaidi ya mara moja na familia yake ilificha ,Alinipiga wakati nina ujauzito, alinipiga ngumi za tumboni na mwili mzima, nilimpoteza mwanangu na bado nilimtetea “ >>>aliandika Kiyomi kupitia ukurasa wake wa twitter kuhusu Bow Wow.
Inaripotiwa kuwa wawili hao walianza mahusiano yao mwaka 2017 na kuripotiwa kuachana February,2019 baada ya kutokea ugomvi kati yao. Bow Wow aliwahi kuwa kwenye uhusiano na Ciara, Keyshia Cole, Erica Mena na Keyomi Leslie na kudaiwa kuwa wote aliachana nao kutokana na kushindwa kuvumilia vurugu zake.
VIDEO: TATHIMINI YA KIKEKE KWA TAIFA STARS, AMUNIKE VIPI AONDOKE?