Baaada ya vingi kuzungumzwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na ndoa kati ya Dogo Janja na Irene Uwoya na kusemekana kuwa imeingia dosari, Irene Uwoya ameonekana kudhihirisha tetesi hizo.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Irene Uwoya amemjibu shabiki anayetumia jina la I am Wailala baada ya kumuambia kuwa ipo siku Dogo Janja atakufa, Irene Uwoya alimjibu na kusema hawezi kufa kwasababu anafata ushauri aliopewa.
Maneno yamekuwa mengi kutokana na Irene Uwoya kutoonekana akiwa karibu na mume wake Dogo Janja, baada ya kulazwa hospitali siku kadhaa zilizopita.
Dogo Janja kaachwa na Irene Uwoya?