Kuna mengi yanaendelea katika michuano ya Kombe la Dunia 2018 kwa sasa na baadhi ya hayo hatupati nafasi ya kuyaona au kusikia, staa wa club ya Watford anayeichezea timu ya taifa ya Morocco Nordin Amrabat ameeleza kutopenda kwa kitendo cha refa kuomba jezi ya Cristiano Ronaldo.
“Sijui kilitokea nini kwa refa lakini alikuwa akimpenda sana Ronaldo na wakati wa mapumziko nilisikia Pepe akisema kuwa refa alikuwa akiomba jezi ya Ronaldo”>>> Nordin Amrabat
Morocco jana alicheza dhidi ya Ureno katika mchezo wa Kundi B wa Kombe la Dunia 2018 na kufungwa kwa goli 1-0, hivyo wachezaji wa Morocco baadhi akiwemo Nordin Amrabat wameoneshwa kutoridhishwa na baadhi ya maamuzi ya refa Mark Geiger.
FULL VIDEO: Zilivyotolewa tuzo za MO Simba Awards 2018