Club ya Yanga leo ilicheza mchezo wake wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania bara uwanja wa Taifa Dar es salaam dhidi ya watani zao Simba SC, mchezo ulimalizika kwa Yanga kupoteza kwa goli 1-0 lililofungwa na Erasto Nyoni dakika ya 37.
Baada ya mambo kwenda mlama kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa alifanya mabadiliko ya kumtoa Papy Tshitshimbi na kumuingiza Emmanuel Martin mabadiliko ambayo mashabiki wa Yanga hawakuyapenda, Nsajigwa ameongea sababu za kumtoa Tshitshimbi kwa sababu alikuwa majeruhi.
VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao