Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars usiku wa June 22 2019 imefanya mazoezi yake ya mwisho kuelekea mchezo wao wa June 23 katika uwanja wa 30 June Cairo, Taifa Stars wanaokipiga dhidi ya Senegal walipata nafasi ya kufanya mazoezi ya mwisho na kuongea na waandishi wa habari.
Nahodha msaidizi wa Taifa Stars Himid Mao baada ya mazoezi hayo aliongea na waandishi wa habari na kueleza kuwa maandalizi yao yapo mazuri na walikuwa wamekaa hapa kwa wiki kadhaa kabla ya michuano kuanza na kwa upande wa watanzania anaomba waendelee kuwaamini kama ilivyokuwa kwenye kufuzu.
“Tumekuja kwenye AFCON ndio nimeongea na wenzangu kuhusiana na hali ya hewa ya hapa lakini pia asilimia kubwa ya timu nyingi hapa ni wageni, kwa hiyo sisi ni wageni na hatuchezi na mtu ambaye yupo nyumbani wote ni wageni chochote kinaweza kutokea japo tunaheshimu kila timu, watanzania naomba waamini chochote kinawezekana kama tumeweza kufuzu na tunaweza kushinda pia”>>> Himid Mao
VIDEO: Okwi baada ya kukabidhiwa tuzo AFCON 2019