Katibu Mkuu wa shirikisho la soka Tanzania TFF Wilfred Kidao leo amekutana na waandishi wa habari nchini na kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusiana na taasisi hiyo, Kidao ameweka wazi pia suala la shirikisho la soka Zanzibar ZFF kudaiwa kuwa halipelekewi mgawo wa pesa kutoka FIFA.
Kidao ameeleza kuwa kwa kawaida pesa za uendeshaji wa taasisi za soka kama TFF zinazotolewa na FIFA kila mwaka kwa mashirikisho wanachama wake huwa zina maelekezo jinsi ya kuzitumia, hazitolewi kama watu wanavyodhani na kingine FIFA imefuta utaratimu wa malipo kwa njia ya pesa taslimu.
“Niwaambia wazi waandishi wa habari haya mambo hayana kificho kuwa FIFA anatoa kiasi gani na anataka mfanye nini kama nchi ndio maana juzi hapa niliona kuna changamoto kuhusiana pesa za FIFA kwa chama cha soka cha Zimbabwe kwa wale waliokuwa wanalalamika mliona majibu kutoka FIFA yalivyokuwa”>>>Wilfred Kidao.
AUDIO:CLUB YA AS ROMA YA ITALIA IMEANZA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI