Taarifa za vurugu zinazo endelea kuripotiwa kutoka Afrika Kusini juu ya raia wenyeji kuwafanyia vurugu raia wakigeni ambao wamekuwa wakiishi nchini humo zimeendelea kuwagusa baadhi ya mastaa na time hii zimemfikia staa kutokea Nigeria ambaye ameonesha kusikitishwa na taarifa hizo.
Peter wa Psquare ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika masikitiko yake na kupinga vitendo hivyo vya vurugu na vya kibaguzi vinavyoendelea dhidi ya raia wakigeni nchini humo.
Peter ameandika haya ….>>>>>
“Moyo wangu unauma kusikia story kuhusu ubaguzi ambao unafanyika Africa kusini. Sisi Africa tutafute namna yakuja pamoja na kutatua hili nchi yetu iwe mahali pazuri kwetu pia na vizazi vyetu. Familia na jamii ni msingi wa kila utamaduni wa kiafrika. Inaniuma sana kuona tuna vurugu sisi kwa sisi bila sababu.
Deni la sasa kwa hali hii uhathirika na heshima kutafuta namna ya kutatua na kumaliza hili jambo lifike mwisho. Nimeamua kusongesha kutoa nyimbo yangu ya kipekee ambayo itawahathiri badae. inatupasa tufanye vyema sisi kama sisi”
ZARI AGUSWA NA VURUGU WANAZOFANYIWA WAGENI AFRIKA KUSINI, KAZUNGUMZA HAYA