Kwa mujibu wa mtandao wa Deadline umeripoti kuwa Rapper Wyclef Jean kutokea nchini Marekani atahusika kwenye utayarishaji wa filamu mpya ikigusia maisha yake ya utoto nchini Haiti.
Rapper huyo atashirikiana na kampuni ya Netflix katika uandaji wa filamu hiyo ikiwa na lengo la kuelezea maisha yake tokea akiwa Haiti na umri wa miaka 9 pamoja na familia yake mpaka kuingia Marekani na kujikita kwenye industry ya muziki.
“Nimekulia kwenye maisha ya umaskini, lakini nimekuwa tajiri kwa ndoto, ili basi kujua hicho nilichokuwa nakiwaza na kikageuka ukweli, mimi na wenzangu tutawaambia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kuwa wasiache kufikia malengo yao” >>>Wyclef Jean
Inaelezwa kuwa filamu hiyo itakayoandaliwa na Wyclef Jean itakuwa katika muundo wa animation(Vikatuni) ili iwafikie watoto ambao wanaishi katika maisha magumu na kuamini katika ndoto zao.
RC Makonda atangaza balaa kwa Mashoga Jiji DSM, Amber Ruthy katajwa